Monday 8 June 2015

Sintofahamu bado yatanda Simba kuhusu Kombe la Kagame

Kikosi-cha-Simba
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba hawana uhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama kombe la Kagame inayoanza kutimua vumbi jijini Dar es salaam Julai 11 mwaka huu.
Awali makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Erick Nyange ‘Kaburu’ alisema watashiriki michuano hiyo sawasawa na kauli iliyotolewa na  TFF kupitia kwa katibu mkuu, Selestine Mwesigwa  kwamba wameichagua Simba badala ya Mbeya City fc wenye uhalali wa kupata nafasi hiyo.
Mwesigwa aliyekaririwa na Mtandao huu alisema Simba wana heshima kubwa, wamekuwa mabingwa mara nyingi wa Kombe la Kagame, hivyo hawawezi kuwatoa.
Lakini leo hii mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema hana uhakika kama watashiriki Kagame kwani mpaka sasa hawana mwaliko rasmi kutoka baraza la soka Afrika mashariki na kati, CECAFA.
“Sidhani kama tutacheza, timu yenyewe hatujaipanga kuanza mazoezi. Hatuwezi kupeleka timu ambayo haijatayarishwa. Kama mpaka sasa hatujapewa mwaliko rasmi, inakuwa tatizo kuanza mazoezi. kama unavyojua kuna wachezaji wengi wapo timu ya taifa, hatuwezi kuingia kwenye mashindano makubwa kama haya kienyeji-enyeji”. Amesema Hans Poppe.

No comments:

Post a Comment

TEAM PARTICIPATING