Kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, tayari amesema jeshi lake lipo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ameuita ni wakusawzisha makosa
USHINDI wa bao 1-0 ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Morogoro wiki iliyopita itakuwa ni moja ya chachu itakayo ipa ari klabu ya Yanga kuutumia vyema uwanja wa taifa Dar es Salaam kuifunga Ndanda FC kesho Jumapili.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake Ndanda FC, ni timu ambayo imeanza kushiriki ligi kuu msimu huu baada ya kushuka kwa timu ya Bandari Mtwara miaka 14 iliyopita.
Ni wazi Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja la kupata ushindi na kujiweka kileleni kwani matokeo mengine yoyote tofauti na ushindi itakuwa imetoa nafasi kwa timu zilizo chini yake kuipita endapo zitashinda mechi zao.
Kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, tayari amesema jeshi lake lipo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ameuita ni wakusawzisha makosa kwa kupata idadi kubwa ya mabao tofauti na mechi iliyopita ambayo wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi na kufunga bao moja.
“Tupo kambini tangu kumaliza mchezo wetu na Polisi Moro vijana wangu wote wapo fiti akiwemo Mrisho Ngasa ambaye hakuwepo kwenye mechi iliyopita kutokana na matatizo ya kifamilia ninaimani tutashinda na kuwafurahisha mashabiki wetu,”amesema Pluijm.
Pluijm amesema anaijuma Ndanda ni moja ya timu ngumu msimu huu hasa inapokuwa inacheza ugenini na anawaheshimu lakini amekianda kikosi chake kwa ajili ya kuchukua ubingwa wa msimu huu na kufanya vizuri michuano ya Kombe la Shirikisha watakayo shiriki baadaye mwezi February.
“Nitaendelea kutumia washambuliaji wawili Danny Mrwanda na Kpah Sherman ambao walifanya vizuri kule Morogoro, wiki iliyopita matumaini yetu ni kupata pointi tatu ambazo zitatufanya tuongoze ligi lakini tukifanana kwa pointi na Azam najua hilo linawezekana ama tutajituma na kucheza kwa bidii zaidi,” ameedelea Pluijm.
“Nimeongea na vijana wangu wamenihakikishia ushindi na uzuri nikwamba kila mchezaji wangu anajua upinzani uliopo kwa sasa kwenye ligi na lengo letu kama tulivyo kubaliana ni kuchukua ubingwa,msimu huu,”amesema.
Pluijm amesema hatokipangua kikosi chake ambacho kilianza Jupili dhidi ya Polisi Moro ambapo golini alimpanga Ally Mustapha ‘Barthez’ Juma Abduli na Oscar Joshua mabeki wa kati alikuwatumia Kelvin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kiungo mkabaji alikuwepo Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima Mrwanda na Kpah Sherman.
Vijana wa kocha Abduli Mingange tayari wamewasili Dar es Salaam wakiwa na matumaini ya kuifunga Yanga kesho na kuendelea kufufua matumaini ya kubaki ligi kuu baada ya wiki iliyopita kupata ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ugenini kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwa kuwafunga Kagera Sugar.
Mingane ameiambia Goal kuwa wanajua mchezo na Yanga ni mgumu kwao lakini watahakikisha wanapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha wanaondoka na ushindi au sare ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.
“Yanga ni timu kubwa na haijafanya vizuri hivi karibuni kwaiyo mchezo utakuwa mgumu kwetu nimewaambia vijana wangu wacheze kwa tahadhari na wasifanye makosa kwenye eneo letu la hatari naamini watafanya hivyo na tutapata matokeo,”amesema Mingange.