Tuesday 16 September 2014

Kavumbagu ampongeza Jaja

Kavumbagu amesema licha ya kupoteza mchezo huo lakini kikosi chao bado ni bora kinauwezo wa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoanza Jumamosi hii.

MSHAMBULIAJI wa Azam raia wa Burundi Didier Kavumbagu,amempongeza mshambuliaji wa Yanga Geilson Santana Santos ‘JAJA’ kwa kufunga bao zuri wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kavumbagu aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Yanga,ameiambia Goal kwamba pamoja na uzembe uliofanya na safu yao ya ulinzi lakini mshambuliaji huyo alifunga mabao mazuri sana na kumpongeza kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha katika ufungaji.

“Nimekubali matokeo tumepoteza mchezo lakini Yule mchezaji mpya wa Yanga amefunga mabao mazuri sana anaonekana jinsi gani alivyokuwa na uwezo anapokuwa mbele ya goli,”anasema Kavumbagu.

Kavumbagu amesema licha ya kupoteza mchezo huo lakini kikosi chao bado ni bora kinauwezo wa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoanza Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment

TEAM PARTICIPATING