Thursday 13 February 2014

Ferguson atafuna boksi 2,500 za Big G uwanjani


Share bookmark Print Email Rating
 


Posted  Jumatano,Novemba7  2012  saa 21:11 PM
Kwa ufupi
Ajengewa mnara Old Trafford wa kuthamini mchango wake
SHARE THIS STORYShar
LONDON, England
MOJA ya sifa ya kocha Sir Alex Ferguson ni kutafuta Big G kama waswahili tulivyozoea kuziita inakadiliwa kocha huyo ameshatafuna maboksi 2,500 hadi sasa.

Idadi hiyo inakadiliwa kutokana uwezo wake wa kutafuna big g 120 katika michezo 60 anayokuwa amekaa kwenye benchi msimu mzima.

Uongozi wa Manchester United katika kuthamini mchango wake hapo tayari imetangaza dhamira ya kutengeneza mnara wa kumbukumbu ya miaka 26, na mafanikio makubwa kutoka kwa kocha huyo raia wa Scotland.

Mnara huo utazinduliwa mwezi huu wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Queens Park Rangers, klabu ambayo kocha huyo aliiongoza United kuanza safari ya mafanikio.

 Takwimu muhimu za maisha ya Ferguson akiwa klabu hiyo ya Old Traffrod zinaonyesha kuwa nusu ya wachezaji alio nao kikosini mwake walikuwa hawajazaliwa wakati alipoanza safari ile.

Hao ni pamoja na kipa David De Gea, mabeki Rafael, Jonny Evans, Phil Jones, Chris Smalling, viungo Anderson, Nick Powell, Tom Cleverley, Shinji Kagawa,washambuliaji  Danny Welbeck na Javier Hernandez, ambao kwa sasa ni baadhi ya nyota ambao wamacheza kikosi cha kwanza cha Man United.

Hakuna shaka kwamba Ferguson amekuwa kocha mwenye mafanikio makubwa ambayo ni vigumu kwa wengi kuyafikia. Amebuni mbinu na kuzitumia kujenga kikosi imara cha muda mrefu.

 Nyota ambao Fergie aliwahi kuwa nao, kisha kuwatimua
Kocha huyo ambaye anatimiza miaka 71  siku ya mwaka mpya, bado anaonekana kama mtu anayeweza kudumu kwa miaka mingine kumi ijayo. Umri wake unamfanya aonekane kama kocha ambaye ni vigumu kufahamu ni lini atatundika daluga na kuiacha United.
Unaweza kujiuliza, ni lini Ferguson anapofikiria kungíatuka? Jibu linapatikana katika kikosi chake ambacho anakijenga msimu huu licha ya kukabiliwa na tatizo katika ulinzi, ingawa amefanikiwa kuiweka United kileleni mwa Ligi Kuu, pia ikiongoza kundi lake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ingawa ana uchungu wa kushindwa kutetea taji msimu uliopita, Ferguson anaeleza kuwa hilo lilitosha kumpa fundisho baada ya wapinzani na jirani zao, Manchester City  kutwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao. Hilo limemtosha Ferguson kufikiria mbinu za kuipa United ubingwa msmu huu na kufikia kilele cha mafanikio katika soka ya England.

Licha ya mafanikio makubwa ambayo yamempa mataji 37,  wazo kuu la uongozi wake akiwa Old Trafford  ni mtazamo wake wa kusaka mafanikio, akiwataka wachezaji wake kusahau yaliyopita na kufikiria mbele waendako .
Huo, ndio umekuwa msimamo wa kocha huyo akiwa United , akiweka kando ndoto za uzee na kufikiria jinsi ya kuipa mafanikio zaidi klabu yake, akieleza kuwa sikuzote hafikirii maisha baada ya kungíatuka soka.
 Mara  kadhaa, Ferguson ametangaza kustaafu, lakini akababili mtazamo na mawazo yake na kuendelea kusaka mafanikio akiwa United.

Mashabiki wengi wa United  wamekuwa wakijiuliza ni lini litatokea  katika maisha ya klabu yao baada ya safari ya Fergie, ingawa yeye binafsi ameweka kando fikra hizo na hata warithi ambao wamekuwa wakitangazwa kuchukua mikoba yake kama vile, Sven Goran Eriksson, kocha aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya England.

Mwaka 2002, kocha huyo alitangaza kustaafu, lakini ghafla akabadili mawazo na kubakia kwa miaka kumi mingine yenye mafanikio na kutwaa mataji matano ya ligi, moja la  Ulaya, jingine la Kombe la FA, matati ya Kombe la Ligi na moja zaidi la klabu bingwa ya dunia.
Kipindi aliposherehekea robo karne ya uongozi wake akiwa United  msimu uliopita, Ferguson alijibu swali  la lini anafikiria kungíatuka kwa kueleza, ìNina miaka miwili au mitatuî zaidi klabuni hapa.

Baada ya kosa la awali la kutangaza kungíatuka kwake, Ferguson aliapa kutorudia tena kosa hilo, jambo ambalo limefanya siri ya lini ataiacha klabu hiyo.

Kwa kutambua ugumu wa kazi ile akiwa United  na aina ya kocha ambaye anafaa kwa kazi ile, mara kadhaa Fergie amesema yeye si mtu wa kupendekeza nani wa kumrithi, ingawa anadhani kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho au Pep Guardiola aliyekuwa Barcelona wanafaa.

Mourinho,  amekuwa na uhusiano mzuri na Ferguson  licha ya upinzani wao kwa ngazi za klabu, zama zile akiwa Chelsea,  bila shaka raia huyo wa ureno anao wasifu ( CV) na mapafu ya kuinoa United baada ya Ferguson kuondoka.

Kocha huyo ametwaa mataji akiwa England, Italia, Ureno na sasa Hispania akiwa na Real Madrid, mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Porto (Ureno),  Inter Milan, Italia, yameboresha wasifu wake kama mrithi anayefaa kwa  Ferguson.

Kwa sasa,  Real Mardid inacheza aina ya soka ya kipekee ambayo haifanini na ile ya Mourinho akiwa Porto, Chelsea na Inter, jambo ambalo linatia hofu mashabiki wa United  endapo ataitwa kwa kazi ya kuinoa United.

Guardiola, kwa upande wake ambaye aliijenga Barcleona , kikosi ambacho Ferguson  alikiri kwamba  ni bora duniani, baada ya kuwashinda katika fainali  mbili za 2009, 2011, pia anapigiwa upatu.
Ferguson na Guardiola,  ambaye hana kazi kwa sasa walikutana New York tangu Septemba wakati ule Fergie akimshangilia mchezaji tenisi  raia wa Scotland,Andy Murray  kwenye michuano ya US Open, ambayo alishinda.
Ni wazi kwamba Guardiola  anabaki mmoja wa watu ambao wanapewa nafasi ya kuvaa viatu vya Fergie na kama kocha huyo atapewa nafasi ya kuteua mrithi.

Sir Alex Ferguson na  Pep Guardiola... je, ndiyo mrithi wake?
Ferguson  anawaona Mourinho na Guardiola, kama vijana wawili makini, ambao angependa kuona mmoja wao akirithi mikoba yake.
Ni dhahiri kwamba Fergie angependa kusherehekea miaka 26 akiwa United kwa kutangazwa kocha bora wa mwezi Oktoba, ikiwa ni mara ya  27 kwake.
Mnara ambao unajengwa nje ya Uwanja wa Old Traffrrod katika eneo lijulikanalo kama Sir Alex Ferguson Stand, jukwaa ambalo awali liliitwa North Stand, utasimikwa  Novemba 23.

Takwimu muhimu za miaka 26 ya Fergie akiwa United
37- Mataji makubwa jumla
12- Mataji ya Ligi Kuu
5- Makombe ya FA
4- Makombe ya Ligi
2- Makombe ya Ulaya
1,461- Mechi alizosimamia United
871- Mechi alizoshinda
260- Mechi alizofungwa
330 ñ Mechi alizotoa sare
2,693- Mabao yote
1,323- Mabao waliyofungwa United
1,988- Pointi za Ligi Kuu
213- Dakika ambazo United imesubiri kufunga bao la kwanza chini ya Ferguson, ushindi wa 1-0  dhidi ya QPR, November 22, 1986
185 ñ Idadi ya wachezaji aliosajili United
45- Rekodi ya mechi ambazo United haikufungwa
9-0 ñ Ushindi mnono wa United dhidi ya  Ipswich, Old Trafford  mwaka 1995
6-1 ñ Kipigo kikubwa cha United dhidi ya  Manchester City  mwaka 2011
Pauni 30.75m  ambazo alilipa kumsajili Dimitar Berbatov mwaka 2008 kwa Spurs
Pauni 80m- Fedha zilizopatikana kwa mauzo ya Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid,  2009
14- Namba ya makocha ambao Man City imekuwa nao wakati Ferguson akiwa United.
17- Mechi  ambazo alizikosa kwa kutumikia adhabu
2,500- Boksi za vitafunwa Big G (chewing gum) ambazo ametafuna Ferguson  wakati wa mechi za  United.
*Ndyesumbilai Florian kwa msaada wa mtandao

No comments:

Post a Comment

TEAM PARTICIPATING